Kikosi cha timu ya Yanga SC kilichoanza dhidi ya Rhino Rangers, katika Dimba la Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans,
leo wameibuka na ushindi na mabao 3 - 0 dhidi ya wenyeji, timu ya Rhino
Rangers katika mchezo uliofanyika jioni katika Uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi mjini Tabora.
Yanga
iliingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi 3 muhimu jambo ambalo
wamefanikiwa na kusogea nyuma ya Azam FC kwa tofauti ya pointi moja.
Ikiwatumia
washambuliaji wake Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Jerrson Tegete na
Emmanuel Okwi safu ya ushambuliaji ya timu ya Young Africans ilikosa
mabao kadhaa ya wazi dakika 20 za mwanzo kutokana na ubovu wa uwanja.
Dakika
ya 29 ya mchezo Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza
baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa timu ya Rhino kufuatia mpira
uliopigwa na Msuva kuokolewa na walinzi wa Rhino kabla ya kumkuta Tegete
aliyeukwamisha mpira wavuni.
Timu
zote ziliendelea kucheza kwa lengo la kusaka mabao kabla ya mapumziko,
lakini mpaka dakika 45 za mchezo zinamalizika, Rhino Rangers 0 - 1 Young
Africans.
Kipindi
cha pili Young Africans waliuanza mchezo kwa kasi na dakika ya 68 ya
mchezo mlinzi wa Rhino Rangers Laban Kambole alijifunga wakati akitaka
kuokoa mpira wa krosi iliyopigwa na Msuva na kuifanya timu ya Young
Africans kuhesabu bao la pili.
Hussein
Javu aliyeingia kuchukua nafasi ya Tegete aliwaiunua mashabiki wa Young
Africans dakika ya 90 o kufuatia kuitumia vizuri pasi ya Okwi
aliyewatoka walinzi wa Rhino na kumpasia Javu aliyeukwamisha mpira
wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamazika, Rhino Rangers 0 - 3 Young Africans.
Baada
ya mchezo wa leo Young Africans inafikisha pointi 43 ikiwa katika
nafasi ya pili nyuma ya Azam FC yenye ponti 44 huku timu zote kwa sasa
zikiwa zimecheza michezo 20 na kubakisha michezo sita kabla ya
kumalizika kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Young Africans: 1.
Juma Kaseja, 2. Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4. Nadir Haroub
"Cannavaro", 5. Kelvin Yondani, 6. Frank Domayo, 7. Saimon Msuva, 8.
Hassan Dilunga, 9. Jerson Tegete/Hussein Javua, 10. Mrisho Ngasa, 11.
Emmanuel Okwi
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL, TABORA)