WAKAZI
wa mjini hapa wamekilaani kitendo cha askari wa kituo kikuu cha polisi
baada ya kumpa kipondo na kumkwida hadi kumvua nguo hadharani dereva wa
daladala aliyefahamika kwa jina la Bello.Tukio hilo lililojaza umati wa
watu lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita ndani ya stendi ya daladala mjini hapa.Mashuhuda wa tukio hilo
walisema Bello aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hiace
inayofanya safari zake kati ya Mjini na Mazimbu, alikamatwa kwa kudaiwa
kuegesha gari vibaya.
“Stendi
ni ndogo Bello aliegesha gari lake akisubiri foleni yake ili apakie, cha
ajabu askari akafika na kumpa kibano kabla ya kumsweka ndani,” alisema
Wamaga Juma na kuongeza:
“Wananchi
wenye hasira walitaka kumzingua askari yule, akapiga simu na kuwaita
wenzake wa kikosi cha usalama barabarani, walipofika walimbeba Bello na
kumpeleka kituoni huku akiwa na kipensi tu.”
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliwapongeza askari hao kwa madai kuwa, madereva wengi wamekuwa wakivunja sheria za barabarani hivyo kibano alichopewa Bello kitakuwa fundisho kwa wengine
