Cristiano Ronaldo amezungumza baada ya kipigo cha jana kutoka FC Barcelona akisema walikuwa wakicheza Barca yenye wachezaji 12.
Mwanasoka
huyo bora wa dunia amesema kwamba refa wa mchezo huo Undiano Mallenco
alichangia timu yake kupoteza wa El Clasico hapo jana usiku katika dimba
la Santiago Bernabeu.
Madrid
walipewa penati ya utata muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza,
lakini Mallenco aliwapa Barca penati mbili muda mfupi baadae — pia
alimtoa kwa kadi nyekundu Sergio Ramos – na Ronaldo anasema anahisi refa
alikuwa akiwapendelea Barcelona kwa makusudi.
