![]() |
| Mkwasa katika picha tofauti jana wakati anaondoka nyumbani kwake. Picha kwa hisani ya mke wa kocha huyo,Betty Mkwasa, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dodoma. |
Wednesday, 19 February 2014
YANGA WAJIBU MAPIGO KWA AL AHLY, SHUSHUSHU LAO CHARLES BONIFACE MKWASA ‘MASTER’ TAYARI LIPO CAIRO
YANGA
SC wamejibu mapigo. Al Ahly walituma wawakilishi wao wiki mbili
zilizopita Dar es Salaam kuja kuangalia timu hiyo ikimenyana na
Komorozine ya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Na
jana kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amepanda ndege
kuelekea Cairo, Misri kushuhudia Al Ahly wakicheza mechi ya Super Cup
dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia, utakaofanyika kesho Uwanja wa Kimataifa
wa Cairo.
Al Ahly walikuja kutazama uchezaji na mbinu za Yanga ambao nao wamemsafirisha Mkwasa Cairo kwa ajili hiyo hiyo.
Mkwasa
anatarajiwa kurejea nchini Ijumaa kuungana na kikosi kwa ajili ya
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting
Jumamosi.
Yanga
SC itamenyana na Al Ahly Machi 1, mwaka huu katika mchezo wa kwanza wa
kuwania kuingia hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
