Thursday, 20 February 2014

Wenger aitaja timu bora kabisa aliyowahi kukutana nayo kwenye maisha ya ufundishaji soka

arsene-wenger_1869548bMasaa kadhaa kabla ya kuingia uwanjani kupmbana na klabu bingwa ya ulaya Bayern Munchen, kocha wa klabu ya Arsene Wenger wapinzani wake wa leo usiku Bayern Munich bado hawana ubora wa kikosi cha Josep Guardiola cha Barcelona kilichobeba ubingwa wa ulaya mara mbili.
Arsenal wanakutana na Bayern katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora, wakiwa na
kumbukumbu ya kutolewa na wajeumani hawa mwaka jana, pia na Barcelona katika misimu ya  2010 na 2011.
Huku Guardiola akiwa meneja mpya wa Bayern, Wenger anasisitiza kwamba hajawahi kucheza na timu ngumu kama ya Barcelona ya chini Guardiola.
“Nilivutiwa mno na Barcelona ilipokuwa kwenye kilele cha ubora wake, kupitia pasi zao na kasi yao ya uwanjani,” Wenger aliambia arsenalfc.com. “Matumaini yangu sitokutana na timu ya namna ile usiku wa leo.
“Mpaka kufikia sasa kwenye maisha yangu, ni timu bora kabisa niliyowahi kucheza dhidi yake ni Barcelona ya Guardiola. Hata sasa bado timu hiyo ni bora, hawajaisha, wameshinda ubingwa wa Spain.
“Bado na wachezaji kama Lionel Messi, Iniesta, Fabregas, na sasa yupo Neymar. Sio wachezaji wa kawaida hawa. Ni wachezaji wa daraja la juu, wana uwezo wa kupambana na yoyote.