Wayne Rooney amedokeza kuwa atasaini Mktaba mpya na Klabu yake Manchester United.Wiki
iliyopita kulivuja habari kuwa Rooney yuko tayari kusaini Mkataba mpya
kuendeleza huu wa sasa unaomalizika mwishoni mwa Msimu ujao na ambao
utakuwa ukimlipa Pauni 300,000 kwa Wiki.
Jana Rooney alitamka kuwa anategemea kuivunja Rekodi ya Ufungaji
Magoli ya Manchester United iliyowekwa na Lejendari Sir Bobby Charlton
nah ii ilileta uthibitisho kuwa atasaini Mkataba mpya.
Rooney alisema: “Siku zote nimesema mie natilia mkazo Soka langu tu na kujaribu kufanya vyema ili Timu iwe na mafanikio!”
Hadi sasa Sir Bobby Charlton ndie Mfungaji Bora wa Man United akiwa na Bao 249 na Rooney amefikisha Bao 208.
Akizungumzia Rekodi hiyo, Rooney alisema: “Kama nitaifikia, nitasikia fahari kubwa kwa sababu ipo kwa muda mrefu!”
Pia zipo fununu kuwa Rooney ndie atakuwa Nahodha mpya wa Man United
baada kuondoka Nemanja Vidic mwishoni mwa Msimu huu kufuatia kumalizika
Mkataba wake.
Wakati
huo huo, Man United inatarajiwa kwenda Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu
mara baada ya Mechi yao na Arsenal hapo Jumatano Usiku kwa Ziara ya
Mazoezi.
Wakati
huo huo, Man United inatarajiwa kwenda Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu
mara baada ya Mechi yao na Arsenal hapo Jumatano Usiku kwa Ziara ya
Mazoezi.
Baada ya Mechi hiyo na Arsenal, Man united hawana Mechi nyingine hadi baada ya Siku 10 watapoivaa Crystal Palace.