Wednesday, 5 February 2014

UN yalaani sera za kanisa katoliki






 


Umoja wa mataifa umetuhumu makao makuu ya kanisa katoliki la Vatican kwa kuidhinisha na kutumia sera zilizowezesha mapadre kubaka na kuwalawiti maelfu ya watoto.

Kamati ya umoja wa mataifa ya haki za watoto imesema kanisa hilo linapaswa kuondoa wote wanaokiuka haki za watoto kutoka nafasi za uongozi na kuanzisha uchunguzi dhidi yao.
Kamati hiyo imekiri kuwa japo Vatican imeshiriki mazungumzo na kuahidi mageuzi, bado inahitaji kupiga hatua kubwa zaidi.
Mengi yaliyoandikwa katika ripoti hii yamekuwa yakiangaziwa na vyombo vya habari. Shutma hizo ni pamoja na kuharibu watoto, kuwapa adhabu kali na kuwatenganisha na wazazi wao.
Umoja wa mataifa unasema uongozi wa kanisa katoliki unapaswa kufanya juhudi zaidi ili kuzuia makosa yaliyowahi kutokea.
Umoja wa mataifa pia umesifia marekebisho yalioyafanywa katika sheria za Vatican lakini umesema kwamba utekelezaji unahitajika kwa kasi.
Kwa upande wake kanisa katoliki limekiri kwamba linahitaji kuhakikisha kwamba sheria zake zinaambatana na sheria za umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto.
Ripoti hiyo pia imekosoa msimamo wa Kanisa katoliki mapenzi ya jinsia moja,upangaji uzazi na uavyaji mimba