Mkazi wa
mmoja wa Nzega, mkoani Tabora, Juma Kiyabo (45) amemchija mke wake,
Wande Monera (34), kabla ya mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi
vibaya shingoni katika jaribio la kutaka kujiua.
Tukio
hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16
mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba
mara kwa mara.
Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kaunga
alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana
na mkewe mara kwa mara kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua
kuchukua hatua hiyo mbaya.
Kamanda
Kaunga alisema kuwa, mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo, naye
alijikata koo kwa lengo la kujiua, lakini hata hivyo jaribio lake
lilishindikana na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.
MWANANCHI