Mshambuliaji
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunguka na kusema kuwa
anajivunia tuzo aliyopewa ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu yake ya TP
Mazembe. Samatta alichaguliwa na mashabiki wa klabu kama mchezaji bora
wa klabu kwa mwaka 2013. Mfungaji huyo bora wa michuano ya kombe la
shirikisho barani Afrika amesema hayo wakati akizungumza na mtandao huu
siku ya leo.
"Nafurahi tu kwa kupata tuzo hiyo, maana wapo wachezaji wengi pia ambao walistahili. Inaleta maana kubwa kama tuzo hiyo inatoka kwa mashabiki wa timu yako."
Samatta
ametokea kuwa mchezaji muhimu sana wa klabu hiyo ambayo aliisaidia
kufika hatua ya fainali ya michuano ya vilabu barani Afrika mwaka
uliopita. Endelea kufuatia mtandao huu ambao kwa sasa upo katika
jitihada za kufanya mahojiano na mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya
Tanzania.
"Nafurahi tu kwa kupata tuzo hiyo, maana wapo wachezaji wengi pia ambao walistahili. Inaleta maana kubwa kama tuzo hiyo inatoka kwa mashabiki wa timu yako."