Kamanda
Mungi alisema kuwa ni ruksa kwa mfanyabiashara yeyote kufungua
biashara yake kwa uhuru na kama kuna mtu atapita kumtisha anapaswa
kupiga simu polisi ili kuchukua hatua kwa watoa vitisho hao . Kwani
alisema ni uhuru wa mfanyabiashara kufungua biashara yake ama
kutofungua na kuwa mtu mwingine asitumie nguvu kumlazizisha
mwingine kufunga ama kufungua. Kamanda Mungi alitangaza namba yake
ya simu kwa ajili ya wafanyabiashara kutoa taarifa pale
wanapotishwa kuwa ni 0754612948 Wakati jeshi la polisi mkoa wa
Iringa likitoa taarifa hiyo ya kuwataka wafanyabiashara kuwa huru
kufungua maduka yao baadhi ya wafanyabiashara eneo la Ipogolo,
Mlandege, Kihesa na katikati ya mitaa ya mji wa Iringa walionyesha
kususia mgomo huo na kuendelea na biashara kama kawaida. Mbali ya
wafanyabiashara hao kugomea mgomo huo kwa madai kuwa kila mmoja
anajua marejesho yake benk ya maeneo mengine bado maeneo ya
uhindini na Miyomboni kwa mara ya kwanza usiku wa leo wafanyabiashara
walioshindwa kufanya biashara mchana walionekana kufungua maduka
yao hadi saa 4 usiku tofauti na siku nyingine ambapo maduka hufungwa
saa 12 hadi saa m |