Wengi waliosikia kuna wimbo wa Shakira na Rihanna unakuja walipata hamu ya kujua muunganiko wa hivi vichwa utakuwaje?Kolabo hii ilipotoka, muda mfupi baadae ilianza kupokea maoni mbalimbali yakiwemo ya kusifia mavazi, muonekano, huku mengine yakihusisha video hii na kampeni ya kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.
Tayari
mwanasiasa maarufu nchini Colombia anakotokea Shakira, Marco Fidel
Ramirez amekua miongoni mwa walioikosoa kwa kutaka mamlaka ya urushaji
wa matangazo ya Television nchini humo iifungie hii video kwa sababu
imekosa maadili, inaonekana kuunga mkono kampeni ya mapenzi ya jinsia
moja.Anasema pia hii video inaweza kushawishi watu wenye udhaifu kuingia kwenye mapenzi ya jinsia moja, ni video ya hatari ambayo pia inachochea matumizi ya tumbaku na vitu vingine vibaya.

Official
video ya huu wimbo iliwekwa wiki moja iliyopita kwenye Vevo account ya
Shakira ambapo mpaka saa tisa usiku wa kuamkia February 8 2014 ilikua
imetazamwa na zaidi ya watu milioni 89 na laki mbili.Hata hivyo hii official video naona imefungwa Youtube ambapo ukiwa Tanzania na nchi nyingine kadhaa huruhusiwi kuitazama.