Wednesday, 12 February 2014

HUYU NDIYE DIAMOND PLATNUM NA MAISHA USIYOYAFAHAMU TANGU AKIWA MTOTO MDOGO, AFANYA KAZI MASAA 8 KIWANDA CHA MABEGI NA KULIPWA SH2,000 TU JIJINI DAR ES SALAAM.

04. Diamond ameshafanya kazi viwandani, Kafanya kazi za kupigisha simu , kuuza mitumba na kuuza maji.
Kuna kipindi Diamond alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi
kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8.
Diamond PlatnumzMambo matano Yatakayokugusa katika maisha ya Diamond Platnumz.
 
01. Diamond Platnumz aliachwa na baba yake
Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam. Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila msaada wowote. Hapa chini huyo ndiyo baba yake diamond.clip_image002

02. Chumba  kupangishwa ili kumsomesha
Baada ya wazazi wake kutengana, Diamond aliamia kwa bibi yake huko tandale na ilipofika muda wa yeye kwenda sekondari ilibidi bibi yake apangishe chumba kimoja ili Diamond aende shule na ikabidi alale chumba kimoja na bibi na mama yake.

03. Aliacha shule kwa kukosa Ada
Diamond alikua na akili darasani na alipomaliza elimu yake ya O’level ilikosekana pesa ya kumpeleka A’level na hapo ndio ilikua mwisho wa elimu yake.

04. Diamond ameshafanya kazi viwandani, Kafanya kazi za kupigisha simu , kuuza mitumba na kuuza maji.
Kuna kipindi Diamond alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8.

05. Mama yake alisaidia sana kutoka kwake
Mama yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza mwanae.