Ukichukulia ukweli kwamba mbwa wako lukuki duniani, huenda msomaji wa safu hii akajiuliza kwamba wapiga picha hao walitembelea sehemu gani na ngapi duniani, wakipiga picha zao, hadi wakafikia uamuzi huo?
Je, waliwahi kufika Nzega au Ifakara (Tanzania), Caracas (Venezuela), Cienfuegos (Cuba) na sehemu zingine mbalimbali duniani wakapiga picha zao na kugundua kwamba mnyama huyo ndiye mbaya zaidi?
Hata hivyo, avumaye baharini ni papa, au mwenye wimbo mzuri huupeleka ngomani. Kwa mujibu wa picha walizopiga watu hao, huenda kweli mbwa mbaya zaidi duniani ni huyu anayeonekana mbele ya macho yako.
Je, mnyama hayu anatisha, anachekesha au “yupo yupo tu?”
Kwa vile hakuna picha zingine za kukinzana na madai ya waliopiga picha hii, basi hakuna budi kila mtu akakubaliana na madai yao kwamba mnyama huyu ndiye mbaya zaidi duniani.