UKISTAAJABU
ya Musa utayaona ya Firauni. Usemi huu unakamilishwa na tukio la
kunaswa kwa vijana wawili wenye undugu wa damu wakifanya mapenzi kando
ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi
Imefahamika kwamba vijana hao, kaka na
dada wamenaswa ‘wakingonoka katika mapango yaliyopo kando ya Ufukwe
wa Coco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Tukio zima lilitokea mchana kweupe wa saa 9 na kudhihirisha habari za mara kwa mara zinazoeleza kwamba Ufukwe wa Coco umekuwa ukitumika kwa ufuska usiku na mchana.
Risasi lilinasa tukio hilo kwa kutumia mitambo maaalum iliyoelekezwa kando ya bahari.
Wawili hao walinaswa tangu walipokuwa wakiingia katika ufukwe huo na kuwafuatilia nyendo zao, hatua kwa hatua.
Haikufahamika mara moja kama wawili hao walikuwa na makubaliano ya kwenda kuduu katika ufukwe huo au la, lakini kwa mbali ilionekana kama vile dada mtu alikuwa akizingua kwenda kutenda dhambi hiyo.
Picha za video zilizonaswa, zinamuonesha dada huyo akionekana kutoa upinzani pale alipokuwa akishikwashikwa na kaka yake.
Alionekana kama vile hakuwa tayari kwa mchezo huo.
Hata hivyo, kaka mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23-26 alikuwa akilazimisha kitu fulani ambacho kilionekana dhahiri kupitia kamera zetu.
Ni kama vile hawakuwa na makubaliano na kile walichokuwa wakienda kukifanya.
Mara
kadhaa dada huyo alionekana kumkwepa kaka yake na alikuwa akijiondoa
karibu yake pale alipomlazimisha kutaka kumfanyia kitu kisichokuwa cha
kawaida
Kamera za Risasi ziliwafuatilia wawili hao kwa kuwa walionekana kuwa na kitu ‘spesho’.
Mpaka wanazama katika mapango yaliyopo kando ya ufukwe huo wa Coco, kamera zilikuwa zikiendelea kuwachukua hadi walipozama ndani kabisa ya mapango hayo.
Walipozama ndani ya mapango hayo, ghafla walitokea askari ambao nao walikuwa wakifuatilia nyendo za wawili hao.
Askari
hao wa Kituo cha Oysterbay, wakiongozwa na kamanda wa oparesheni
maalumu katika Wilaya ya Kinondoni, Kamanda Swai walifuatilia kwa
umakini tukio hilo.
Wakiwa
chini ya mapango, kaka na dada waliondoa vinguo vilivyokuwa maungoni
mwao na kuanza kuduu kama vile walikuwa katika ufukwe unaoruhusiwa
kufanya vitendo hivyo.
Kabla askari hawajawavamia, waliwashuhudia wawili hao wakiwa katika kilele cha sterehe yao huku dada mtu akionesha kutoa ushirikiano kwa shingo upande.
Ghafla, askari waliwavamia na kuwatibulia starehe yao kisha kuwatia mbaroni.
Baada
ya kuona kuwa wamevamiwa na askari, kaka mtu alichomoka na kutafuta
silaha ili kuweza kujihami na wavamizi wake bila ya kujua kama ni
askari.
Katika
hilo nusura zipigwe kati ya askari na kaka huyo ambaye alikuwa akitaka
kupigana na watu asiowajua kwa kuwa walikuwa wametinga mavazi ya kiraia.
Hata hivyo, alitulizwa na kutakiwa kuvaa pensi yake ili aweze kutoa maelezo kwa kina.
Wakati
yote yakiendelea, dada mtu alikuwa amepigwa na butwaa na kutojua cha
kufanya hadi aliporushiwa kitenge chake kilichokuwa pembeni ili
ajisitiri mwili wake.
Katika mahojiano ya awali yaliyoongozwa na Kamanda Swai, ilibainika kwamba wawili hao ni ndugu wa damu yaani kaka na dada.
Maelezo
hayo yanasema kuwa dada mtu alitoka mkoani na alikuja kutembea jijini
Dar es Salaam, ndipo kaka yake alipomtaka watoke kwenda kumuonesha
vivutio vya jiji hilo.
“Nina
miaka 19, nimetokea Iringa kuja Dar kutembelea familia lakini kaka
akanileta huku na kunifanyia vile, siyo kama tulikuwa tumekubaliana,”
alisema dada huyo kwa aibu.
Kaka mtu alikiri kile kilichosemwa na dada yake na kushindwa kujitetea kwa kuwa kila kitu kilikuwa hadharani.
Wawili hao walichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Oysterbay kwa ajili ya kufunguliwa kesi ya uzembe na uzururaji na kusekwa rumande kabla ya kufikishwa