Tuesday, 4 February 2014
Juliana Shonza Anena na kugawa Dozi Mtandaoni
Jina mbwa koko ni maarufu miongoni mwa waswahili wa nchi hii. Aghalabu neno hilo kutumika katika majukwaa ya kisiasa lakin kiuhalisia neno hilo linafanana sana baadhi ya watu wanaofanya siasa hapa nchini. Mfanano huo ni wa kitabia, hivyo kufanya watu hao kushabihiana na mbwa koko. Tabia hizo ni kama zifuatazo.
(I) Mbwa koko huwa wanatabia ya kubweka bila kufanya lolote.
(II) Mbwa koko ni waoga, uwingi wao hauna maana wala msingi, mmoja wao akipigwa wemgine hufyata mkia na kukimbia hovyo. Hawana ujasiri.
(III) Mbwa koko ni viumbe vinavyotangatanga, hawana makazi wala malazi. Hawana uhakika na maisha yao wala kesho yao.
Hizo ndizo tabia tatu kuu za mbwa koko. Ama ile ya kwanza ya kubweka bila kuwa na uwezo wa kufanya lolote ndio tabia kuu na maarufu ya mbwa koko wote duniani. Utawasikia wakati mwingine wakitishia jambo ambalo hawana uwezo nalo, wanaweza kutishia utawala wa nchi, kuwa hautakuwa salama, mara wanaweza kutishia kikundi cha watu kama wasanii kuwa hawatauza kazi zao na kiuhalisia hawana meno wala uwezo wa kufanya lolote katika yale wanayotishia kuyafanya.
tabia ya pili ya uoga, nayo ndio silaha kuu ya mbwa koko viongozi, wanawatisha wafuasi wao na kuwafanya wawe wanachama wafuata mkumbo, wanawatia ujinga na kuwafanya wapoteze ujasiri wa kuhoji chochote.
tabia ya tatu ya mbwa koko ni kutangatanga, aah ulahi wa aah ulahi. Hapa hawapo wala pale hawapo. Hawana msimamo hawana mwelekeo. Wapo wapo tu. Hawana itikadi, hawana sera, hawana katiba. Analosema mbwa koko kiongozi ndio msahafu hakuna anayepinga wala kuhoji. Leo wanadandia hoja hii kesho wanaamka na hoja nyingine.
AMA tukiachana na mbwa koko;
Kuna hili suala lililoibuka hivi karibun kuhusu wasanii waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) hivi karibuni. Wapo waliowabeza na hata kuwatisha kuwa hawatanunua kazi zao na kuwakwamisha katika tasnia yao. Nasema huu ni umbumbumbu, kwani ni msanii gani wa kwao wao ama aliowaunga mkono wao na mauzo yake yakaongezeka kwa kuwa kajiunga na wao, nani alifanya show nyingi zilizomlipa mamilioni baada ya kutangaza kuwa ni wa itikadi yao. Ama msanii gani ambaye hata anachukuliwa na kuzunguka nao katika mikutano yao hata waseme wao wanawajali wasanii kuliko wengine. Ni ujinga.