Tuesday, 4 February 2014

HILI NDO JENGO REFU KULIKO YOTE DUNIANI..ANGALIA PICHA NA VIDEO

 NewsImages/3861786.jpg




Jengo refu kuliko yote duniani lililopo Dubai ambalo limeenda angani mita 828 toka ardhini linalojulikana kama Burj Khalifa



Jengo hilo ambalo awali lilikuwa likijulikana kama Burj Dubai
kabla ya Dubai kupewa msaada wa kifedha na Abu Dhabi baada ya kuingia kwenye madeni, lilifunguliwa kwa sherehe iliyoambatana na shoo ya fataki mbali mbali.

Jengo hilo lilibadilishwa jina na kuitwa Burj Khalifa ili kumuenzi kiongozi wa Abu Dhabi aliyeipa msaada Dubai wa dola bilioni 10.

Jengo hilo lina urefu wa mita 828 na lina ghorofa 160 ambazo ni nyingi sana kulinganisha na jengo lililokuwa likijulikana awali kama ndilo refu kuliko yote duniani la Taipei lenye ghorofa 101.

Ghorofa hilo ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2004, mbali ya kuwa jengo refu kuliko yote duniani ndilo pia jengo lenye lifti ndefu kuliko zote duniani.

Jengo hilo pia lina msikiti ulio juu kuliko yote duniani kwenye ghorofa ya 158 na lina bwawa kubwa la kuogelea lililo juu kuliko yote duniani kwenye ghorofa ya 76.