Filbert Bayi, 1974
Jumapili
ya February 2, Filbert Bayi ametimiza miaka 40 tangu avunje rekodi ya
dunia ya mita 1500, katika mashindano ya jumuiya ya madola.
Hata
hivyo, rekodi hiyo ambayo hadi leo haijawahi kuvunjwa kwenye mashindano
hayo imeonekana kusahaulika duniani na hiyo inamuumiza Bayi. Bayi
alimaliza mbio hizo kwa dakika 3 na sekunde 32.16, February 2, 1974,
huko Christchurch, New Zealand na hadi leo yeye ndio mkimbiaji bora
zaidi wa urefu huo kuwahi kutokea duniani.
Katika
mbio hizo, Bayi alimzidi John Walker aliyekamata nafasi ya pili, nafasi
ya tatu ikaenda kwa Ben Jipcho wa Kenya, ya nne kwa Rod Dixon wa New
Zealand na ya tano kwa Graham Crouch wa Australia. Bayi, pia alishinda
medali ya fedha ya mbio za 3000m za Moscow Olympics mwaka 1980.