Sehemu ya masalia ya bati na matandiko yalio haribiwa na mvua
SACAP
Deusdedit Kamugisha Afisa wa Magereza Mkoa wa Iringa pichani kulia
akiongozana na Mkuu wa gereza Pawaga SP.Sosthenes Mwakapala akikagua
uharibifu ulio jitokeza katika nyumba za askari na majengo wanayo
tarajia kuhamia kwamuda.
Bustani ikiwa imeharibiwa na Mvua ilionyesha ikiwa na upepo mkari
Baadhi ya Vyombo vya familia za Askari Magereza vikiwa nje baada ya Mvua kuharibu makazi yao.
Nyumba
kumi na tano za Askari Magereza wa Gereza Pawaga wilaya ya Iringa
zimeezuliwa na Upepo mkali ulio ambatana na mvua kubwa ya mawe
ilionyesha juzi majira ya saa 9 alasiri mpaka saa kumi na moja jioni na
kuanza tena saa mbili ya usiku mpaka saa tano usiku.
Akiongea
na mwandishi wa habari Mkuu wa Gereza la Pawaga SP.Sosthenes Mwakapala
alisema adha hiyo ya mvua imesababisha familia hizo kukosa mahala pa
kuishi pamoja na thamani zilizo salia wakati walipokumbwa na mvua hiyo
ingawa hakuna madhara kwa binadamu sambamba na hilo kumeezuliwa ofisi za
tano za gereza zinazojumuisha Stoo, Bohari, Mapokezi, Utawara pia Bafu
ya wafungwa.
Madhara
mengine yaliyo jitokeza ni kuharibiwa vibaya kwa heka tano za Bustani ya
gereza yenye mazao mchanganyiko ikiwamo mashina ya Ndizi, Mipapai,
Mihogo, Mahindi pamoja na Miwa mimea hiyo imevunjika kabisa
haitegemewi kupona tena.
Mkuu
wagareza la Pawaga SP. Sosthenes Mwakapala alisema wao kama uongozi
wagereza na viongozi wasaidizi wake wamechukua jukumu la kuhakikisha
askari hao na familia zao wanapata mahali pakujihifadhi kwa muda wakati
wakisubiri ufumbuzi toka ofisi ya Magereza mkoa wa Iringa.
Kwakuwahamishia katika majengo ya Shule ya Msingi, Bwalo la gereza,
Ghala la chakula wakae kwa muda.na mjengwa blog