MREMBO
anayedaiwa kuliingilia penzi la staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki Shindano la Miss
Tanzania, Amisa Mabeto amefunguka kuwa mwanamuziki huyo ni shemeji yake
tu, hakuna chochote kati yao.
Akipiga
stori na safu hii kuhusiana na madai hayo, Amisa alisema alistaajabu
kwani hana mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi kuonana miaka ya
nyuma, tena siyo kimapenzi.
“Kamwe
siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo
na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa, siwezi
kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu,” alisema Amisa.


