Tuesday, 18 February 2014

CHADEMA YACHUKUA FOMU YA KUGOMBAEA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

1_ad5e8.jpg
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalenga Bi Pudensiana Kisaka akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Kalenga Bi. Grace Tendega anayeiwakilisha CHADEMA katika ukumbi wa sayansi na kilimo cha wilaya ya Iringa vijijini leo hii.
2_604e3.jpg
kiongozi huyo wa CHADEMA alipokuwa anawasili katika eneo la ukumbi huo kwenda kuchukua fomu hiyo ambayo kwa mujibu ya sheria za uchaguzi huo inatakiwa kurudishwa tarehe 18/02/2014 (kesho, Jumanne) 
ANGALIA PICHA ZAIDI
3_bda39.jpg
msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo la Kalenga; Bi. Pudensiana Kisaka alipokuwa anamkaribisha kiongozi huyo wa CHADEMA, Bi. Grace Tendega kuchukua fomu hiyo katika ukumbi huo.
4_8c786.jpg
Bi. Grace Tendega alipokuwa anakaribia kukabidhiwa fomu hiyo ya ugombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la Kalenga kupitia CHADEMA 
5_22974.jpg
6_d3145.jpg
wajumbe wa CHADEMA waliohudhuria tukio hilo leo. 
7_d2768.jpg
Kiongozi huyo (Grace Tendega) alipokuwa katika ofisi ya  CHADEMA wilaya ya Iringa katika eneo la Mshindo; alipokuwa akijibu maswali waandishi wa habari.
Na Riziki Mashaka.