MBUNGE
wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amekamatwa na polisi
kufuatia vurugu kubwa zilizoibuka leo katika uchaguzi mdogo wa
udiwani kata ya Nduli jimbo la Iringa mjini baada ya wafuasi wa chama
cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kuwashambulia wafuasi wa CCM .
Tukio
hilo limetokea jioni ya leo baada ya wafuasi wa Chadema
kuwashambulia kwa mawe na nondo wafuasi wa CCM na kupelekea kijana
mmoja wa UVCCM Salum Kaita kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika
Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa .
Wakizungumzia
tukio hilo baadhi ya mashuhuda waliozungumza na mtandao huu wa matukio
daima walidai kuwa Chadema walikuwa na mkutano eneo la Nduli na
vijana hao wa CCM walikuwa mbali na eneo la mkutano wakiendelea na
shughuli zao kabla ya kuvamiwa na makada wa Chadema.
Hata
hivyo wakati wa vurugu hizo zikitokea inadaiwa mbunge Msigwa
alikuwa akishuhudia tukio zima na kutuhumiwa kuhusika kufanya njama
za kuwashambulia vijana hao.
Naibu
meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki amemweleza mwandishi wa
habari hizi kuwa ana sauti ya mbunge Msigwa inayoelezea jinsi
ambavyo mbunge huyo alivyopanga kufanyika kwa vurugu hizo.
Huku
mmoja kati ya makada wa Chadema mjini hapa akidai kuwa CCM ndio
ambao walihusika na vurugu hizo kutokana na kupita eneo hilo la
mkutano wa Chadema wakati wao hawakuwa na ratiba ya kufanya mkutano
eneo hilo.
Mwandishi
wa habari hizi ameshuhudia askari wa FFU mkoa wa Iringa
wakiwaongoza wafuasi wa Chadema zaidi ya 20 waliokuwa katika gari
la matangazo pamoja na mbunge Msigwa ambae alikuwa chini ya ulinzi na
kufika kituoni hapo kwa gari lake la ubunge .
Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi hakuweza kupatikana
kuelezea undani wa tukio hilo na jitihada za kumtafuta zinaendelea
japo hadi sasa saa moja hii usiku mbunge Msigwa yupo kituo cha
polisi akihojiwa
CHANZO: MATUKIODAIMA.COM
|