Story
hii ilitoka February 15 ambayo ilitolewa na Jeshi la Polisi Mtwara
kuhusu kukamatwa kwa watu watatu ambao walikuwa wakisafirisha pembe za
ndovu zenye thamani ya Milion 700,kutoka Mtwara kuja Dar es
salaam,walikamatwa alfajiri ya February 14 saa 11 katika kijiji cha
Chungu kata ya Nanyumbu, tarafa ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara.
Millardayo.com
imepata picha za Gari hiyo aina ya Toyota Land Cruiser,jinsi jamaa
walivyotoboa hapo nyuma sehemu ya kukaa abiria,watuhumiwa hao walikua na
jumla ya meno 58 yenye uzito wa jumla ya kilo 130.6 waliyapakiza kwenye
gari aina ya Toyota Land cruiser T208 AGC.Hizi ndizo picha za Gari hiyo.





