Dunia
haiishi vituko! Chacha Makenge (36) mzaliwa wa Kijiji cha Kisangula,
Mtukula, Serengeti mkoani Mara anaishi jijini Dar lakini ndani ya
handaki aliloligeuza chumba kwa miaka minne sasa, ni ajabu lakini ni
kweli.Akizungumza
na mwandishi wetu hivi karibuni nje ya handaki hilo lililopo mita
chache kutoka majengo ya biashara ya Mlimani City, Makenge alisema
alichukua uamuzi huo baada ya rafiki yake (jina linahifadhiwa) kumchomea
nyumba na kuteketeza samani zote.
“Ilikuwa
mwaka 2009 mwanzoni rafiki yangu huyo ndiye alinipa sehemu ya kiwanja
chake nijenge nyumba. Nikawa naishi hapo huku nikiendelea na shughuli
zangu za kila siku.
“Siku moja akabadili mawazo, akanitaka nihame katika eneo lake bila kunipa sababu, nilimwomba anipe muda nitafute pa kwenda.
“Julai 2009 akaja na polisi, akanikamata na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Stakishari, nilipowauliza kosa langu, hawakunieleza.
“Baada
ya siku mbili majirani walikuja kuniona na kuniambia kwamba nyumba
yangu imechomwa moto na kila kitu kilichokuwa ndani kimeteketea,
aliyefanya hivyo ni rafiki yangu. Nilijisikia vibaya sana.
“Siku
iliyofuata majirani walikuja tena kituoni wakaniwekea dhamana.
Nilipofika kwangu nilikuta majivu tu, iliniuma sana, nililia lakini
sikupata ufumbuzi. Kwa vile nilikuwa sina pa kwenda ilibidi niwe nalala
palepale nilipochomewa nyumba nikisaidiwa chakula na majirani.
“Siku
iliyofuata, saa nne usiku nilivamiwa na watu wanne, wakiwa na mapanga
na marungu, nilipambana nao mpaka wakaondoka. Kesho yake nilikwenda kwa
mwenyekiti wetu wa serikali ya mtaa, Jumanne Malima kumweleza
yaliyonipata, alisikitika, akaniandikia barua kwenda Polisi Stakishari.
“Nilipofika
kituoni sikusikilizwa, badala yake walinikamata tena na kuniweka ndani
wakidai kwamba nimefunguliwa kesi ya kumjeruhi mtu kwa panga.
Hawakukubali niwekewe dhamana.
“Julai
31, 2009 nilifikishwa Mahakama ya Mwanzo Ukonga na baadaye nilipelekwa
Mahabusu ya Gereza la Keko, nikawa napelekwa mahakamani hadi Septemba
mwaka huo ambako nilihukumiwa kwenda jela miezi 9.
“Nilitumikia
maisha ya jela hadi Desemba 10, 2009 nikatolewa kwa msamaha wa Rais
Jakaya Kikwete. Nilikwenda kuishi kwa ndugu zangu huku wakifuatilia
sababu ya kufanyiwa vitendo hivyo bila mafanikio.
“Maisha
ya kwa ndugu hayakunifurahisha kwani hata wao walikuwa na majukumu
mengi, niliamua kuendelea na kazi zangu za sanaa pia utunzaji wa
mazingira na bustani kwa watu wakawa wananilipa fedha.
“Ndipo
nilipoamua kutafuta sehemu iliyotulia ili niweze kuishi, nikapata hapa,
ni jirani na Mlimani City. Nilichimba handaki kubwa kama unavyoliona,
kwa chini kuna kitanda ninacholalia.
“Kwa
hakika hapa sipati shida, wala kelele. Kwanza ni tulivu sana, nimefikia
hatua ya kuishi kama mnyama kutokana na mateso na bugudha nilizopata,
wengi hawajui nilipo, nipo katika pori hili kwa miaka minne
sasa,”alisema Makenge.CHANZO GPL