![]() |
| Mtuhumiwa Dorah Joseph (34). |
Kwa mujibu wa majirani na mashuhuda,
kisa cha mwanamke huyo kufanya kitendo hicho cha kikatili, ni katika
harakati zake za kutaka kumtumia mtoto huyo kishirikina ili aweze
kujipatia mali.
Akizungumza muda mfupi baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo
ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Eleray
alisema shangazi yake huyo amekuwa akimfanyia ukatili wa kutisha
akishirikiana na jirani yake ambaye jina lake linahifadhiwa.
![]() |
Mtoto Happy Joseph (13).
‘’Shangazi ananitesa sana,
ananifunga mnyororo kama mbwa na kunifungia chumbani, hanipi chakula
wala kunipeleka shule, nina zaidi ya mwaka sasa sijaenda,” alidai Happy.
Aliongeza kuwa tofauti na dada yake, yeye ndiye amekuwa akiteswa huku ndugu zake wakizuiwa kumuona.
Akizungumzia tukio hilo, Askari wa Dawati la Jinsia, Deborah alisema
ukatili uliofanywa na dada huyo kwa mwanafunzi huyo hauelezeki na kwamba
wanakamilisha mashtaka ili kumfikisha mahakamani ili liwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa
huyo na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye hadi anafikishwa polisi,
alikuwa bado na mnyororo mguuni kutokana na kukosekekana kwa ufunguo wa
kufungua kufuli kubwa mguuni kwake.
Kwa upande wake, mtuhumiwa huyo alisema alilazimika kumfunga mnyororo
binti huyo baada ya kuchoshwa na tabia yake ya kuzurura ovyo, kwani
muda mwingi anatoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana.
Alisema mara kadhaa mtoto huyo amekuwa akitoweka nyumbani hapo wakati
mwingine kwa wiki nzima bila kujulikana alikoelekea, ikiwa ni pamoja na
kutoroka shuleni.

