Denis Mtima, aliyekuwa Igunga, Tabora
KWA mara ya kwanza, mzazi mwenza na msanii wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shilole’, Elias Makala ameibuka na kujinadi hadharani wilayani Igunga,
Tabora.KWA mara ya kwanza, mzazi mwenza na msanii wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed
Tukio hilo lilitokea
Februari 14, mwaka huu (Valentine’s Day) ambapo Shilole aliyekuwa amekwenda
kufanya shoo mkoani humo, alishindwa kuzuia hisia zake baada ya mzazi mwenzake
huyo kujitokeza na kujikuta wakioneshana mahaba mbele za watu.
Pozi hilo la kimahaba
liliwashangaza watu na kuanza kudhani kuwa huenda wawili hao wakarudisha penzi
lao lililokufa miaka mingi iliyopita.
“Mh! Kweli mtalaka
hatongozwi, hebu ona Shilole alivyorembua alipomuona jamaa yake, pale Makala
kumchukua ni kama kumsukuma mlevi,” alisema shuhuda mmoja.
Baada ya paparazi wetu
‘kuusoma mchezo’ huo, aliamua kumuuliza staa huyo kama penzi lao limerudi upya
au laa?
“Hahahahaa! Kwa kweli
unanichekesha kuniuliza kama nimerudisha penzi kwa mzazi mwenzangu, huyu ni
baba wa mwanangu Joyce, itabaki kuwa hivyo. Siwezi kumtenga na sioni ajabu
kupiga naye picha, hakuna kinachoendelea,’’ alisema Shilole.
Licha ya kufafanua hivyo,
usiku wa siku hiyo, Shilole alipokuwa jukwaani akipagawisha mashabiki kwa shoo
kali, alimpandisha jukwaani mzazi mwenziye huyo hali iliyozua mtafaruku mkubwa
kwa mpenzi wa sasa wa Makala aliyefahamika kwa jina la Maguno.
Baada ya shoo kuisha,
Maguno aliyekuwa na jazba kwa mpenzi wake kupandishwa jukwaani, alimsaka
Shilole kwa udi na uvumba kutaka kumtembezea kichapo lakini bahati haikuwa
yake, hakuweza kumpata hadi msanii huyo aliporejea jijini Dar siku iliyofuata.
-GPL
