Ripoti
mpya iliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) inaonyesha Watanzania milioni
4.2 wanaishi chini ya mstari wa umaskini kwa kupata Sh886 kwa siku.
Ripoti hiyo inabainisha kuwa Watanzania hao ambao wanaishi mijini na
vijijini, wanapata Sh26,000 kwa mwezi, ambayo ni sawa na Sh866 kwa siku.
Akizindua Toleo la Nne la Taarifa ya Hali ya Uchumi nchini jijini Dar es
Salaam juzi, Mkurugenzi wa WB, Philippe Dongier alisema hali hiyo
inatisha.
Dongier alisema mpango huo ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa nchi za Brazil
na Mexico na kwamba, nchini umetekelezwa wilaya za Bagamoyo, Kibaha na
Chamwino kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
Mtaalamu wa Uchumi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi na
Uganda, Jacques Morisset alisema asilimia 18.7 ya wananchi wanaoishi
mijini ni maskini, huku vijijini wakichukua asilimia 71.2.
Aliongeza kuwa asilimia moja ya wakazi wa Dar es Salaam, ni maskini wa kupindukia.
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu Kitengo cha Kuratibu Utendaji Ofisi ya Rais
(PDB), Peniel Lyimo alisema siyo vyema kwa watu kujadili kama Tanzania
inaweza kuondoa umaskini uliokithiri au la, badala yake waamini kwamba
hali hiyo itakwisha nchini.
“Kwa namna ambavyo Serikali inatoa mchango mkubwa kwenye kilimo, hasa
kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) umaskini uliopindukia
utakwisha,” alisema Lyimo.
Naye Meneja wa Sera za Uchumi wa WB kwa nchi za Maziwa Makuu, Albert
Zeufack alisema nchi nyingi zimeingia katika umaskini kutokana na tabia
ya Serikali zao kupenda kukopa fedha nyingi hasa wakati wa uchaguzi mkuu
kwenye nchi zao