Kamishna wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule akizungumza na wanahabari ofisini kwake baada ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu 11 wilayani Rombo
Afisa wa uhamiaji wilaya ya Rombo akiwasindikiza watu wawili ambao wanatuhumiwa kuwa ndio wahusika wa usafirishaji wa wahamiaji haramu hao.
Bi. Leokadia Tarimo raia wa Tanzania na Bw. Paulo Endevayesu raia wa Burundi ambao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu hao
Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Rombo katika moja ya nyumba ya wageni.
Askari wakiwa katika gari lililopeba wahamiaji haramu hao waliokamatwa wilayani Rombo katika moja ya nyumba ya wageni.
a Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.
Kwa hisani ya Michuzi Blog
a Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.
WIMBI la wahamiaji haramu kuingia nchini limeendelea kushika kasi
katika siku za karibuni kufuatia kukamatwa kwa wahamiaji haramu
wengine 11 raia wa Ethiopia katika kijiji cha Mlele kata ya Mashati
wilayani Rombo wakiwa wamehifadhiwa katika nyumba ya kulala wageni.
Tukio la kukamatwa kwa wahamiaji hao linakuja ikiwa ni wiki moja
imepita baada ya kukamatwa kwa kundi jingine kubwa la wahamiaji haramu
wapatao 56 katika kijiji cha Jiungeni wilayani Same wakiwa katika
harakati za kufanya safari kuelekea nchini Afrika Kusini kwa lengo la
kutafuta kazi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amesema kuwa wahamiaji hao walikamatwa juzi majira ya saa 7 mchana baada ya
askari polisi waliokuwa doria kupata taarifa ya kuwepo kwa wahamiaji
hao haramu katika moja ya nyumba za wageni.
“Jana(Juzi) saa 7 mchana askari wakiwa doria walipata taarifa kuwa
kuna wahamiaji haramu na kwamba kwamba wamefichwa kwenye nyumba moja
katika kijiji cha mlele kata ya Mashati na askari baada ya kufika
katika nyumba hiyo waliwakuta”alisema Kamanda Boaz.
Alisema baada ya kukamatwa kwa wahamiaji hao polisi ilianza
ufuatiliaji juu ya wahusika waliowaingiza nchini na kuwahifadhi ndipo
wakafanikiwa kumkamata mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la
Leocadia Gapiti ambaye anadaiwa kuwa ndiye mmiliki wa nyumba hiyo.
“Tumemkamata mwanamke mmoja anaitwa Leokadia Gapiti ambaye alikuwa
amewahifadhi kwenye nyumba hiyo na mwingine Paulo Endevayesu ambaye
ndiye wakala halisi ambaye alikuwa anawasafirisha watu hao.”alisema.
Kamanda
Boaz alisema uchunguzi zaidi unafanyika ili kujua watu hao walikuwa
wanatoka wapi wanaenda wapi na kwamba pindi utakapo kamilika
watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Kwa upande wake kamishna msaidizi wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Bw.
Johanes Msumule alisema wamebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa katika
suala hilo na kwamba tayari wanaendelea kuwahoji watu wawili
waliokamatwa ambao ni Leokadia na Paulo Endevayesu raia wa Burundi.
Alisema katika kipindi cha wiki tatu kilichopita tayari wamesafirishwa
zaidi ya wahamiaji haramu 74 kurudi nchini mwao Ethiopia ambapo kundi la
kwanza lilikuwa la wahamiaji haramu 18 ambao walikabidhiwa kwa askari
wa Kenya .
Alisema kundi la pili lilikuwa la wahamiaji haramu 56 lililokamatwa
hivi karibuni lilisafirshwa hivi karibuni kupitia mpaka wa Namanga
hadi katika kijiji cha Moyale kilichopo mpakani ma nchi za Kenya na
Ethiopia.
Tukio la karibuni lilihusisha kukamatwa kwa wahabeshi 56 katika kijiji
cha Jiungeni –Same wakiwa katika Lori aina ya Fuso, yenye namba za
usajili, T188 AYU,linalotajwa kama mali ya kampuni ya ELyimo Trans ya
Mjini Moshi likiwa na jina la Godbless Mbasha wa mkoani Manyara.