Thursday, 19 December 2013

TASWIRA ZA AJALI YA BASI LA HOOD ILIYOUA MMOJA NA KUJERUHI 27 MKOANI MORO LEO

Wananchi wakilishuhudia basi la Hood baada ya kupinduka eneo la Melela-Mlandizi, Mvomero mkoani Morogoro.
Gari hilo baada ya kupinduka.
Baadhi ya abiria wakitoa mizigo yao katika basi hilo.
Baadhi ya abiria waliokuwa wanasafiri katika basi hilo.
Basi hilo likitolewa eneo la ajali.
...Baada ya kutolewa.
Baadhi ya wananchi wakipanda basi lingine la Hood kuendelea na safari kama kawaida.
Eneo la Melela Mlandizi ilipotokea ajali hiyo.
BASI la kampuni ya Hood Limited aina ya Scania lenye namba za usajili T 159 AXM lililokuwa likitoka jijini Mbeya kueleka Arusha limepinduka kwenye kona kali iliyopo eneo la Melela, Mlandizi wilayani Mvomero, Morogoro leo majira ya saa nane mchana na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi 27.
Majeruhi kadhaa katika ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu.
Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kwamba chanzo chake ni dereva wa lori aliyejaribu kulipita gari lingine kwenye kona hiyo.
"Mimi nilikuwa natoka Mbeya naenda Moshi kwa ajli ya sikukuu ya Krismas, dereva wetu amefanya kazi kubwa sana ya kuokoa maisha yetu.
"Tulipofika hapa kwenye kona, dereva wetu baada ya kuona lori limejaa upande wetu akaamua kukwepa kugongana nalo uso kwa uso na kuingia huku lilipo. Binafsi nampa pongezi nyingi dereva wa hili basi letu" alisema Bi. Ruth Mwambogoso abiria katika basi hilo
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MORORGORO)