Monday, 23 December 2013

MPANDA: MBOWE ASHINDWA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA

Katika hali isyotarajiwa Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh.Mbowe jana alishindwa kufanya mkutano wa hadhara kutokana na hali ya sintofahamu iliyojitokeza kwenye mkutano wa ndani uliofanyika kwenye ukumbi wa St.Marry's Mjini Mpanda.
 
Hiii ni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa vijana wengi kwenye chama hicho hawamtaki Mbunge wao Mh.Said Arfi,Mbunge wa viti maalum Anna Malack na katibu wa Mbunge Bw.Joseph Mona kutokana na kutowajibika pia kitendo cha Bw.Arfi kutupa kadi ya CDM kwenye mkutano wao uliofanyika huko Nkasi hali iliyosababisha Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Rukwa kufukuzwa kwenye nyadhifa yake.

Vijana walikwenda mbali zaidi na kumtaka Mbowe atoe tamko la kumkataa Mh.Arfi na aondolewe kwenye chama kwani ni msaliti na hawamtaki kabisa. 
 
Mh.Mbowe alishindwa kutoa maamuzi magumu na kuliweka kiporo jambo hilo.
 
Mkutano ulifika hadi saa 4 usiku hivyo kupelekea mkutano wa hadhara kwa siku ya jana usifanyike.
 


Jamii Forums post by  Wakurogwa