Mbunge wa jimbo la Isimani ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi kulia akimkabidhi msaada wa gari la wagonjwa mganga mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Ignesa Mlowe kwa ajili ya kituo cha afya Kimande gari lenye thamani ya Tsh milioni 180 lililotolewa na serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii
Mbunge wa jimbo la Isimani ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi akimkabidhi msaada wa fedha kiasi cha Tsh milioni 2.2 kwa ajili ya kusafisha mfereji wa umwagiliaji anayepokea kulia ni mwenyekiti wa jumuiya ya wakulima wea mpunga katika mfereji wa Mlenge Bw Fundi Maleva leo
Mbunge wa jimbo la Isimani ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi akijaribu pikipiki mbili zilizotolewa na rais Dr Jakaya kikwete kwa jumuiya ya watumiaji maji Pawaga .
MBUNGE wa jimbo la Isimani mkoani Iringa Wiliama Lukuvi amekabidhi gari la wagonjwa lenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 180 kwa kituo cha afya Kimande Pawaga na kumwondoa aliyekuwa dereva wa gari la awali ambaye alituhumiwa kupakia meno ya tembo katika gari la wangonjwa.
Hata hivyo alisema kuwa hakuna mwenye uhakika na tuhuma za dereva huyo kujihusisha na kitendo cha kubeba meno ya tembo kupitia gari la wagonjwa kama ambavyo moja kati ya magazeti hapa nchini yalipata kutoa tuhuma hizo kwa dereva huyo.
"Nimeamua kutumia busara zaidi kumwondoa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo la wagonjwa na kumweka mwingine kutokana na upotoshwaji uliofanywa na moja kati ya magazeti kwa kuandika kuwa dereva huyo anabeba meno ya tembo katika gari hilo ....japo tambueni kuwa sifa mbaya si kwa dereva ni kwa wananchi wote wa tarafa ya pawaga ila tumemleta dereva mwingine"
Huku akimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutekeleza ahadi yake ya pikipiki na ujenzi wa majengo ya jumuiya ya watumiaji maji pamoja na kutoka usafiri wa pikipiki wa viongozi wa jumuiya hiyo.Akizungumza leo na wananchi wa tarafa ya Pawaga baada ya kukabidhi msaada wa gari hilo la wagonjwa ambalo limetolewa na wizara ya afya , Lukuvi alisema kuwa magari kama hayo yametolewa katika maeneo mbali mbali ya nchi na katika mkoa wa Iringa ni gari moja pekee ndilo limetolewa kwa wananchi wa Pawaga.
Hata hivyo alisema kuwa anampongeza waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr Husein Mwinyi ambae alifika katika eneo hilo akiwa naibu waziri wa afya na kuahidi kutatua kero ya vifo vya wanawake wajawazito ambavyo vilikuwa vikitokea kutokana na eneo hilo kukosa gari la wagonjwa .
Kuhusu huduma ya maji katika eneo la Mlenge alisema kuwa kiasi cha Tsh bilioni 2 zinahitajika kwa ajili ya wananchi wa eneo hilo la Mlenge ambao kwa sasa hawanahuduma ya maji.
Alisema jumuiya ya watumiaji maji ya Pawaga inayonafasi ya kutumia vema mradi huo wa maji ili ikiwezekano kuwezesha wananchi wa jirani na kijiji hicho kuweza kupata huduma ya maji na kuwa wasisite kuwachukulia hatua wafugaji jamii ya kimasai na wasukuma ambao wameendelea kuhujumu miundo mbinu ya maji kwa kukata mabomba ya maji.
Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge alisema kuwa ndoto yake ya maendeleo katika jimbo hilo hasa pawaga ni kuona wananchi wa eneo hilo wanaunganishwa na barabara ya uhakika na badala ya kwenda mjini Iringa kupata usafiri sasa wakatengenezewa barabara itakayounganisha eneo hilo na barabara ya Iringa- Dodoma.
Alisema kuwa zipo fedha ambazo zimetolewa na ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kuwa na barabara za mfano kwa ajili ya kuinua uchumi wa wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo katika mradi huo watahakikisha wanajenga ghara la kuhifadhia mazao ya wakulima hasa zao la mpunga.
Lukuvi alisema kuwa timu ya wataalam itafika katika eneo la Pawaga ili kutoa elimu kwa wakulima wa mpunga ili kuboresha zaidi kilimo na soko la mchele wao kupitia mradi huo ambao umetengewa fedha na ofisi ya waziri mkuu.
Wakati huo huo Lukuvi amekabidhi msaada wa Tsh milioni 2.2 kwa wakulima wanaotumia mfereji wa umwagiliaji wa Mlenge ili mtambo wa kusafisha mfereji huo baada ya kuombwa na wananchi hao wa tarafa ya pawaga