Sunday, 15 December 2013

MAHAFALI YA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA IAA: KILIO CHA RUSHWA CHAZIDI KUITESHA SERIKALI

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Goodluck Ole-Medeye (katikati), akiongoza wahitimu wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kuelekea kwenye viwanja vya chuo hicho, muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti kwenye fani mbalimbali mkoani humo mwishoni mwa wiki, wa kwanza ( kushoto) ni Mkuu wa Chuo hicho Prof Johannes Monyo, na Mwenyekiti wa Bodi ya uongozi wa (IAA), Mwanaidi Mtanda.
Wahitimu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakivaa kofia zao muda mfupi baada ya kutunukiwa vyeti vya fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo, kwenye sherehe za mahafali ya 15 zilizofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mwishoni mwa wiki.

Kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ubinafsi ndani ya idara na taasisi za serikali nchini kumeelezwa kuwa ni chanzo na ‘mwiba’ unaorudisha nyuma juhudi na mipango madhubuti inayofanywa kila siku na serikali dhidi ya wimbi la umasikini

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Goodluck Ole-Medeye, ameyasema hayo mkoani hapa, mwishoni mwa wiki, wakati akihutubia kwenye  sherehe za mahafali ya 15 ya Chuo cha Uhasibu Arusha

“Sehemu ya fedha za walipakodi huishia kwenye midomo ya walafi wachache ambao baadhi yao ni  viongozi wasio waadilifu wenye dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo ya taifa letu ,”  alisema Medeye na kuongeza.