Mwanaume
raia wa China ambaye alipata ajali ya kukatwa kabisa mkono wake wa
kulia na mashine ya kiwandani, alilazimika kuunganishwa mkono huo na
kifundo cha cha mguu wake (ankle) kwa muda wa mwezi mzima ili uendelee
kuwa hai wakati akisubiri kufanyiwa upasuaji wa kurudishiwa mkono huo
sehemu yake.
Madaktari waliomhudumia Xiao mara baada ya kupata ajali hiyo Novemba 10, walimwambia hawataweza kuuokoa mkono wake, lakini alipohamishiwa katika hospitali kubwa masaa saba baada ya ajali ndipo alipoambiwa bado kuna uwezekano wa mkono huo uliotengana kabisa kuwa hai.
Xiao
aliambiwa zoezi la kuurudisha mkono wake sehemu yake linaweza
kufanikiwa, lakini mpaka mkono wake wa kulia utakapopona kabisa. Na ili
kuendelea kuufanya mkono uliokatika uwe hai wakati huo wa kusubiri,
madaktari walisema hawana njia nyingine zaidi ya kuunganisha na ‘ankle’
ya mguu wake.
Desemba
10 ndipo madaktari waliamua kuurudisha mkono wa Xiao sehemu yake, na
wamesema kuwa zoezi la upasuaji huo lilienda vizuri japo kuwa
atahitajika kufanyiwa operations nyingi za ziada ili kuufanya mkono
upone kabisa.
Source: The Independent