HIVI NDIVYO JINSI NDEGE YA ETHIOPIA AIRLINE ILIVYOCHIMBA UWANJA WA NDEGE ARUSHA BAADA YA KUTUA GHAFLA,IKIWA NA ABIRIA 200
Muonekano wa ndege ya Ethiopian Airline baada ya kutua kwa dharura.
Watu 200 waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya
Ethiopian Airline wanusurika kufa baada ya ndege kupitiliza hadi nje ya
uwanja mdogo wa ndege wa Arusha baada ya kutua kwa dharura.
Ndege
aina ya Boeing 767 inayosadikiwa kuwa ni ya Shirika la Ndege la
Ethiopia imetua kwa dharura majira ya saa tisa alasiri katika kiwanja
cha kurushia ndege ndogo cha Arusha badala ya kiwanja cha ndege cha
Kimataifa cha Kilimanjaro, KIA. Abiria
zaidi ya mia mbili waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamenusurika kifo,
wanasubiri msaada ngazi waweze kushushwa._Picha na Dj sek Blog