![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfYLEi2jc3GluX8wE2PhJ-65GWXpU_OJgeRHLpBwpgAqmHjev-AK9tTqxdaFyekC5x0r0AIPaBxgt6VgX1Sw5USQpGuZFoxwOU4HFyT6a3sbo6IG0Q0D9bJ-eJcDdAqpb-NWoqgcevRNg/s1600/article-2569367-1A60658200000578-91_634x406.jpg)
Maelfu
ya saini za mashabiki wa soka zimekusanywa katika ombi rasmi la kutaka
kiungo wa Manchester United Tom Cleverley kufungiwa kucheza katika
michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Brazil mwaka huu.
Mpaka
sasa ombi hilo limeshakusanya jumla ya saini 6,000 ndani ya kipindi cha
masaa 36, lilikusanya saini 4,000 ndani ya masaa 24, na lilosomeka kama
ifuatavyo: 'Tom Cleverley, ambaye tayari ameshaichezea England mechi
13, amekuwa akiteuliwa na Roy Hodgson katika vikosi vya England bila
kuwa na sifa yoyote ya maana.
'Tunaamini
katika taswira nzuri ya kikosi cha taifa hili kubwa na kwamba tunataka
azuiwe kushiriki katika michuano ijayo ya kombe la dunia.
'England
inaaminika kuwa ni timu mbovu katika michuano mikubwa, hivyo aibu zaidi
inaweza kuepukika kwa kutomjumuisha yeye na kiwango dhaifu
kitachoshusha jitihada za timu nzima.'
Kama
ilivyo kwa wachezaji wenzie wengi, Cleverley ameshindwa kurudia kiwango
chake kizuri alichokuwa nacho miaka miwili iliyopita, kilichomfanya Sir
Alex Ferguson kumuita 'special player'
Cleverley
amefunga goli moja tu katika michezo 32 aliyoichezea klabu yake na
amekuwa akisemwa mpaka na mashabiki wa timu yake, hasa kwenye mtandao wa
Twitter.