Mrisho
Khalfan Ngassa jana alifunga tena mabao matatu peke yake katika ushindi
wa 5-2 wa Yanga dhidi ya wenyeji Komorozine ya Comoro katika mchezo wa
marudiano, Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Ngassa ambaye pia
alifunga hat trick wakati Yanga inaichapa mabao 7-0 Komorozine katika
mchezo wa kwanza Dar es
Salaam, ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba mabao yake
yote hayo amzawadia mwanamuziki rafiki yake kipenzi, Diamond pichani
kulia, kwa sababu alimtabiri atafunga idadi hiyo ya mabao kabla ya mechi
hiyo. Ngassa na Diamond ni marafiki walioshibana na wamewahi kufanya
tangazo la biashara pamoja
source-binzuberi