NYOTA
wawili wa Arsenal, Per Mertesacker na Tomas Rosicky wamekubali kusaini
mikataba mipya ya kuendelea kupiga kazi Uwanja wa Emirates.
BIN
ZUBEIRY inafahamu The Gunners imekuwa ikiwatongoza wachezaji hao
kuongeza mikataba tangu Septemba mwaka jana - na sasa klabu hiyo ya Ligi
Kuu ya England imethibitisha wachezaji hao wanabaki.
Mertesacker
ametweet picha akiwa kijana mdogo amevaa jezi ya Arsenal na kuandika
maelezo: "Tangu nikiwa mdogo hadi sasa, najivunia kuwa gunner! Asante
mashabiki kwaa sapoti yenu. Furaha kuongeza muda na @Arsenal.
![]() |
| Bado yupo sana; Beki Mjerumani Per Martersacker ameongeza Mkataba Arsenal hadi mwaka 2017 |
Wanabaki: Rosicky na Mertesacker wameongeza mikataba yao Emirates
"Tuna furaha kwamba Mertesacker na Rosicky wamejifunga mustakabali wao katika klabu,"amesema kocha Arsene Wenger.
Kiungo
wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, Rosicky amesaini Mkataba wa miezi 12
zaidi wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja na ataendelea kulipwa
Pauni 80,000 kwa wiki.
Beki
la kimataifa la Ujerumani, Mertesacker inafahamika amesaini mkataba wa
miaka mitatu na nusu, utakaokwenda hadi mwaka 2017. Lakini yeye mkataba
wake mpya ataongezewa mshahara kutoka Pauni 80,000 kwa wiki anazolipwa
sasa.
Mtutu mdogo: Per Mertesacker ametweet picha yake akiwa mdogo amevaa jezi ya Arsenal baada ya kukubali kusaini mkataba mpya
