MSHAMBULIAJI
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu sasa amekuwa
Mchungaji wa kanisa moja la kilokole nchini Marekani, imeelezwa.
Rafiki
mmoja wa karibu Nteze, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Nteze
aliyewika Pamba FC ya Mwanza na Simba SC ya Dar es Salaam, kwa sasa
amekuwa mtumishi wa Mungu baada ya kustaafu soka.
Nteze
aliibukia Pamba FC mwaka 1990 na mwaka 1994 akasajiliwa Simba SC hadi
alipokwenda Afrika Kusini na Marekani kucheza soka ya kulipwa.
Nteze alirejea Simba SC mwaka 2002 na baada ya hapo akatungika daluga zake na kwenda kuishi Marekani.
Nteze ni kati ya wanasoka wachache waliopata mafanikio wakiwa na klabu na timu za taifa pia.
Kwani
pamoja na kushinda mataji mawili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, sasa Kombe la Kagame akiwa na Simba SC mwaka 1995 na 2002, pia
alishinda Kombe la CECAFA Challenge mwaka 1994 akiwa na timu ya Bara,
Kilimanjaro Stars nchini Kenya na Kombe la CECAFA Castle mwaka 2001
mjini Mwanza akiwa na Taifa Stars.

