Kwa
mujibu wa mtandao wa Bongo5, Makamba na Sugu wameshiriki kwenye wimbo
wa hip hop uliowahusisha rappers 13 wa Tanzania, wimbo wenye lengo la
kusisitiza sanaa kutambulika kwenye katiba mpya. Katika wimbo huo,
January Makamba amefanya Intro na Outro imefanywa na Sugu.
Rappers
walioshiriki kwenye wimbo huo uliopewa jina la ‘Haki’ ni Kala Jeremiah,
Quck Rocker, G-Nako, Nikki wa Pili, Mwana Fa, Danny Msimamo, Profesa
Jay, Gosby, Joh Makini, Fid Q na Kala Pina.
‘Haki’ imetayarishwa ndani ya Bongo Records na mtayarishaji mkongwe P-Funk Majani.
Kwa
mujibu wa John Kitime, mwanamuziki mkongwe wa Tanzania, wasanii
wamepanga kuwa na kikao na waandishi wa habari (press conference) na
kuzindua wimbo huo.