KADIRI siku zinavyokwenda kumekuwapo na ugunduzi wa vitu mbalimbali vinavyochangia kuleta mabadiliko katika jamii.
Mabadiliko hayo yanaweza kuwa hasi au chanya kutegemea na aina ya bidhaa iliyogunduliwa na matumizi yake.
Zipo
bidhaa zinazoonekana kuwa na matokeo ya haraka na mazuri baada ya
kutumika, lakini wakati huo huo kuwa na madhara kiafya kwa mtumiaji.
Nchi
nyingi zinazoendelea hasa zilizopo barani Afrika ikiwamo Tanzania
zimekuwa ndizo waathirika wakubwa wa bidhaa zinaotajwa kuwa na madhara
huku vijana wakiwa ndiyo kundi kubwa linaloathirika. Sababu za kundi
hilo kuathirika zaidi ni kutaka kwenda na wakati kwa kujaribu kutumia
kila bidhaa zinazotoka nje ya nchi bila kujua madhara yake.
Miongoni
mwa bidhaa hizo ni nguo za ndani zilizoundwa maalumu kwa ajili ya
kupunguza unene, pia kutengeneza umbile la mvaaji katika mwonekano wenye
mvuto aupendao. Nguo hizo zimetengenezwa kwa mtindo wa mbano, (Skin
tight)ambapo ikivaliwa hubana eneo la tumboni hadi kwenye mapaja na
hufanya kazi ya kupunguza unene, zikiufanya mwili kuwa mwembamba
kulingana na nguo husika ilivyo.
Licha
ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kusaidia kwa kiasi kikubwa watu
wengi kupunguza miili yao, utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa nguo
hizo za ndani huchangia kwa kiwango kikubwa uwezekano wa mvaaji kupata
matatizo ya kiafya.
Utafiti
uliofanywa na wataalamu mbalimbali wa nchini Uingereza, unaonyesha kuwa
uvaaji wa nguo hizo unaweza kumfanya mvaaji kupata maradhi ya mgongo,
saratani na kiwango kikubwa cha asidi mwilini.
Mmoja
wa wataalamu wa afya katika Hospitali ya The London Clinic, Dk Johnson
Wilson, anasema kubana kwa nguo hizo katika eneo la tumbo huzuia
mzunguko wa asidi inayozalishwa ndani ya mwili na kuisababisha kupanda
juu, badala ya kushuka chini.
Anasema
kuwa hali hiyo inatokana na msukomo unaotokea kwenye tumbo, hivyo
kusababisha mlundikano wa asidi ndani ya mwili ambayo hupaswa kutoka
baada ya kuzalishwa.
“Nguo
hii inapovaliwa inatenganisha eneo la kifuani na tumbo, hivyo asidi
inayozalishwa inashindwa kushuka chini na matokeo yake inashia kwenya
usawa wa matiti na kurudi kwenye mrija unaopitisha chakula,”anasema
DkWilson.
Kuhusu
hatari ya saratani, Dk Wilson anasema kuwa kulundikana kwa asidi katika
mrija wa chakula, kunamweka mhusika katika hatari ya kupata saratani ya
koo na kinywa.
Anasema
kwamba licha ya kuwa siyo watu wengi walioathirika na uvaaji wa nguo
hizo, lakini matokea yake huonekana baada ya muda mrefu kutokana muda
ambao mhusika atavaa nguo hizo.
“Hatari
ipo zaidi kwa wanaovaa nguo hizi mara kwa mara, madhara yake hayawezi
kuonekana kwa haraka zaidi, lakini kiafya kuna hatari ya kutengeneza
saratani ya koo kutokana na kuzuia asidi na kusababishia irudi na
kulundikana kwenye mrija unaosafirisha chakula,”anaonya.
Pamoja
na hatari hiyo uvaaji wa nguo hizoi pia unachangia kusababisha ugonjwa
wa ngozi unaotokana na mwili kubanwa kupita kiasi, hivyo hewa kushindwa
kupita.
Dk
Wilson anafafanua kuwa ikifikia hatua hiyo, kuna uwezekano wa
kutengeneza mazingira ya bakteria na fangasi kujificha kwenye mwili
hivyo kusababisha mvaaji kupata maradhi ya ngozi yaliyo magumu kutibika.
Mtaalamu
wa ngozi Dk Sam Bunting anasema, kubanwa kwa ngozi pamoja na joto
linalosababishwa na msuguano, vinachangia kuleta madhara makubwa katika
mwili wa binadamu.
“Hali
hii inasababisha ugonjwa unaofahamika kwa jina la kitaalamu kama
Intertirgo, ambao huwatokea watu wanaovaa nguo maalumu za kubana kwa
ajili ya kutengeneza maumbile,”anasema.
Nguo
hizo pia huchangia kuifanya misuli ya tumbo kuwa dhaifu, kutokana na
kubanwa muda mwingi, hata inapoachwa huru inashindwa kuwa na nguvu yake
ya kawaida.
“Kwa
asili misuli ya tumbo haina nguvu na unapoibana kwa muda mrefu
unaisababishia kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi, hivyo hulegea na
kuwa dhaifu zaidi hata inapofunguliwa au kutolewa nguo
inayobana,”anasema.
Kwa
upande mwingine, mtaalamu wa misuli Dk Robert Shanks anasema kuwa nguo
hizo zinachangia pia kusababisha maumivu ya mgongo kwa mvaaji. Anasema
nguo hiyo inapovaliwa, kunakuwapo na ugumu kwa viungo vya mgongo
kujongea kwa urahisi, hivyo kusababisha maumivu ya mgongo mara kwa mara.
“Viungo
na mifupa iliyopo kwenye mgongo inapaswa kujongea, lakini kuibana
kupita kiasi kutasababisha kushindikana kwa hali hiyo hivyo mvaaji
lazima atakumbana na maumivu ya mgongo mara kwa mara”
Pamoja
na madhara hayo, nguo hizi pia huweza kusababisha kizuizi katika
mzunguko wa damu kwani mishipa inayotakiwa kufanyakazi hiyo inashindwa,
kutokana na maeneo ya tumbo hadi kwenye nyonga yanakuwa yamebanwa.
“Ni
vigumu mzunguko wa damu kufanyika vizuri katika maeneo yaliyobanwa
kupita kiasi; ni wazi kuwa nguo hizi siyo rafiki, huifanya damu
isizunguke inavyopaswa,”anasema Dk Shanks na kuongeza:
“Ikifikia
hatua hiyo, kuna dalili mvaaji kuweza kupata maimivu ya miguu kwa kuwa
mishipa ya damu iliyopo katika maeneo hayo inashindwa kufanya kazi yake
vizuri.”
Kwa
upande wake mtaalamu wa masuala ya ngozi nchini Tanzania, Dk Isack
Maro, anasema kuwa madhara yanayotokana na uvaaji huo siyo makubwa
ikilinganishwa na ripoti ya utafiti unavyoeleza.
“Inawezekana
kukawapo uwezekeno wa kupata maradhi ya ngozi kutokana na mwili kubanwa
kwa muda mrefu, hivyo jasho kushindwa kutoka na kutengeneza mazingira
ya fangasi,”anasema Dk Maro na kuongeza:
“Madhara
yapo, lakini siyo kwa ukubwa huo. Inawezekana kuwakumba watu wachache
mno kati ya wengi, lakini sidhani kama yanaweza kuwa kwa ukubwa
