WAGONJWA WASUBIRI KUTAMBULIWA NA NDUGU ZAO HOSPITALINI MUHIMBILI
KAMERA
yetu jana ilitembelea Taasisi ya Tiba na Mifupa na Mishipa ya Fahamu
(MOI), wodi za Sewahaji na Maisela vyumba namba 17 na 18 katika
hospitali ya Muhimbili na kugundua kuna wagonjwa kadhaa ambao aidha
wametelekezwa na ndugu zao au hawafahamu kwamba wana ndugu zao katika
hospitali hiyo.
Katika kuwahoji, wagonjwa hao walitoa wito kwa watu wanaowafahamu kuwasaidia kufikisha kilio chao kwa ndugu zao.