Monday, 6 January 2014

BreakingNEWS: Sababu Kesi ya Zitto Kuahirishwa mpaka Kesho Hii Hapa



Zitto Kabwe Kushoto akiwa na wakili wake, Albert Msando wakitoka Katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, wiki iliyopita siku ya kwanza alipofungua kesi katika mahakama hiyo.
Dar es Salaam, Tanzania.Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha kutoan uamuzi HIVI PUNDE na sasa hukumu hiyo itatolewa kesho, saa 8:00 mchana.
Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, kesi hiyo imeahirishwa mpaka kesho mchana kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hiyo hajamaliza kuandika hukumu ya kesi hiyo. 

Nje ya mahakama, wafuasi na wanachama wa Chadema wanaimba nyimbo zinazomgusa Zitto.

"Hahaa Zitto akifaa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera kiwe chakula cha mambaaa x2

Kwa upande mwingine, LEO Zitto hakifika katika mahakamani bali aliefika ni wakili wake, Albert Msando.
Awali iliripotiwa kwa makosa kwamba alikuwapo mahakamini.
Watu ni wengi.

Waandishi wa habari wapo hapa geti la mahakama.
Nje ya mahakama wafuasi wa Chadema na wale wa Zitto walikuwa wakirushiana maneno ya hapa na pale huku wafuasi wa Zitto wakiimba "Zitto ni mkombozi x2" pia wafuasi wa Zitto walikuwa na ngoma.

Vile vile wafuasi wa Chadema nao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali kumponda Zitto.

Leo wafuasi wa Chadema na Zitto hawakupiga kama Ijumaa iliyopita kwani ulinzi ulikuwa mkali sana.

Wengine walipoona ulinzi walikimbilia mitaani hasa waliokuwa wakijaribu kurusha ma