Hatimaye lile sekeseke la ndoa ya
meneja wa wasanii wa Bongo Fleva wanaosimamiwa na Kampuni ya Endless
Fame, Petit Man na mdogo wa
mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz limemdondokea Wema Isaac Sepetu anayedaiwa kuitibua kiasi cha kuwatenganisha na kila mmoja kuchukua hamsini zake.
Habari
kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, Wema amehusika kwa asilimia kubwa
kutibua ndoa hiyo kwani amekuwa akimtafutia mademu Petit Man, jambo
ambalo Esma alilishtukia na kuamua kumbwatukia Wema kwa kuandika maneno
makali kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa taarifa yenu Esma anamlalamikia Wema kuwa anamfanya mumewe kuwa mhuni kiasi kwamba anachukua mademu, tena marafiki zake na hata akimuuliza Petit Man anajifanya hao ni mashoga wa Wema.“Anapomkomalia, mara kadhaa umekuwa ukizuka ugomvi mkubwa na Petit Man anahama nyumbani kwake na kukimbilia kwa Wema,” kilisema chanzo chetu.Baada ya kunyetishiwa ‘infomesheni’ hizo, gazeti hili liliingia kazini kusaka ukweli wa mambo yanayodaiwa juu ya
lilianzia
kwa Esma, alipopatikana alisema ni kweli hivi karibuni aliandika ujumbe
kwenye Mtandao wa Instagram, ingawa kwenye maelezo yake hakumtaja mtu
bali aliandika kwa hisia kama binadamu mwingine anavyoweza kuandika.
“Nani anasema nimemtukana mtu? Niliandika mambo ambayo nilijisikia mwenyewe lakini sikumtaja wala kumlenga mtu yeyote, kama kuna mtu alikwazika basi atakuwa anajichanganya mwenyewe.“Mimi sina tatizo na Wema na mambo ya familia yangu siwezi kumwambia kila mtu hivyo kama kuna ugomvi kati yangu na mume wangu hayo ni mambo ya familia yetu,” alisema Esma.
Kwa upande wake Wema alifunguka kwamba hajawahi kuongea jambo na Esma na kama kuna kitu aliandika kwenye ‘peji’ yake yeye hakuona.Alisema anachokumbuka ni kwamba aliongea naye (Esma) akiwa Hospitali ya Aga Khan Aghakan, Dar.
“Huwa siongei na Esma mara kwa mara kwani sina sababu sana ya kuwa naye kwa kuwa si mume wala bwana’ngu.
“Pia sijawahi kukwaruzana naye, sasa kama kuna kitu alisema, mimi namtafutia wanawake mumewe basi atakuwa anakosea kabisa,” alisema Wema