MECHI
ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza
sh. 448,414,000.
Mapato
hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia
pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh.
35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219,
waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.
Uwanja
sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.
