Timu
ya Yanga leo wameibuka kidedea kwa kuizamisha Al Ahly bao moja kwa bila
katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo ni ya raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa Afrika. Mfungaji
wa Yanga ni Nadir Haroub "Cannavaro" katika dakika ya 82 kipindi cha
pili.