Madereva
wa malori zaidi ya mia tatu wamegoma kuendelea na safari katika
barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza baada ya dereva mwezao aliyekuwa
akiendesha lori kuvamiwa na majambazi katika eneo la kisaki manispaa ya
Singida.
Wakiongea
na ITV /Radio one madereva ambao wamekutwa katika eneo hilo wameomba
jeshi la polisi kufanya doria mara kwa mara eneo hilo kwani kumekuwa na
matuki yanayo jirudia ya utekeji wa magari kwa kuweka mawe makubwa
barabarani na kuwajeruhi madereva jambo ambalo lina tishia amani kwa
watumiaji wa barabara.
Madereva
wa malori baada ya kufunga barabara naibu waziri wa Afrika mashariki
Dr. Abdulla Abdulla alikumbwa na adha hiyo na kusema ni haki ya kikatiba
kwa madereva kugoma kwa kudai haki zao, kutokana na hali hiyo
amewahaidi madereva kupeleka kilio chao katika mamlaka husika ili kuweza
kutatua tatizo lao na kukomesha vitendo vya uvamizi wa magari katika
eneo hilo .
Kwa
upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP Geofrey
Kamwela amesema madereva waliamua kusimama barabarani bila sababu yeyote
kwa muda wa zaidi ya masaa matatu na kusababisha foleni kubwa ambapo
kwamujibu wa sheria za usalama barabarani walikuwa wamefanya kosa
,lakini baada ya viongozi kufika na kuwasikiliza waliamua kuendelea na
safari.
Naye
dereva wa lori bwana Agustino Mbawala aliye tekwa, akiwa amelazwa
katika hospitali ya mkoa wa Singida akiongea kwa shida huku akiwa na
maumivu makali amesema aliona mawe makubwa barabarani na kuamua kusimama
na kukimbia lakini wali mvamia na kumpiga hatimaye kumpora fedha na
simu