Bilioni 3? Etoile du Sahel inataka Euro Milioni 1.3 sawa na Sh. Bilioni 3.1 kutoka SC Villa ilyomuuza Emmanuel Okwi Yanga SC |
Saturday, 1 March 2014
ETOILE SASA WATAKA KULIPWA BILIONI 3.1 ISHU YA OKWI, WAPO KIZIMBANI FIFA LEO
ETOILE
Sportive du Sahel ya Tunisia imefufua kesi ya mshambuliaji wa kimataifa
wa Yanga, Mganda, Emmanuel Okwi, Shirikisho la Soka la Kimataifa
(FIFA), safari hii ikitaka kulipwa fidia ya Euro Milioni 1.5 sawa na Sh.
Bilioni 3.1 za Tanzania.
Kwa
mujibu wa habari kutoka Zurich, Usiswi makao makuu ya FIFA, E.S.S.
wanakwenda Zurich leo kujadili suala la mchezaji huyo wakiwa tayari
wamesema wanataka walipwe Euro Milioni 1.5.
Lakini E.S.S. inataka fedha hizo zilipwe na klabu ya SC Villa ya Uganda, ambayo ilimuuza mchezaji huyo Yanga SC.
“Wanakwenda
leo Zurich kujadili suala hili, wameitaka FIFA kuiagiza klabu ya
Uganda, kulipa Euro Milioni 1.3 kutoka sehemu ya fedha walizopata kwa
kumuuza mchezaji huyo Yanga SC,”kimesema chanzo kutoka FIFA.
Ikumbukwe
Okwi alisajiliwa Etoile akitokea Simba SC ya jijini Dar es Salaam tangu
Januari 2013 kwa dau la Dola za Kimarekani 300,000 zaidi ya Sh. Milioni
480 za Tanzania.
Hata
hivyo, baada ya miezi mitatu mchezaji huyo aliingia kwenye mgogoro na
klabu hiyo ya Tunisia, Etoile ikimtuhumu Okwi kuchelewa kurejea kazini
baada ya ruhusa ya kwenda kuitumikia timu yaTaifa ya Uganda (Uganda
Cranes).
Okwi
aliyapangua madai hayo kwa kusema klabu hiyo ilishindwa kumlipa
mishahara kwa miezi mitatu mfululizo na akafanikiwa kuishawishi FIFA
imruhusu kujiunga na SC Villa ili kulinda kiwango chake wakati suala
lake likitafutiwa ufumbuzi.
Hata
hivyo, Desemba mwaka jana Villa ikamuuza Okwi Yanga SC ambapo
ameidhinishwa kuendelea na kazi, huku Etoile ikiifufua kesi hiyo.