Jana Rooney alitamka kuwa anategemea kuivunja Rekodi ya Ufungaji
Magoli ya Manchester United iliyowekwa na Lejendari Sir Bobby Charlton
nah ii ilileta uthibitisho kuwa atasaini Mkataba mpya.
Hadi sasa Sir Bobby Charlton ndie Mfungaji Bora wa Man United akiwa na Bao 249 na Rooney amefikisha Bao 208.
Akizungumzia Rekodi hiyo, Rooney alisema: “Kama nitaifikia, nitasikia fahari kubwa kwa sababu ipo kwa muda mrefu!”
Pia zipo fununu kuwa Rooney ndie atakuwa Nahodha mpya wa Man United
baada kuondoka Nemanja Vidic mwishoni mwa Msimu huu kufuatia kumalizika
Mkataba wake.
Wakati
huo huo, Man United inatarajiwa kwenda Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu
mara baada ya Mechi yao na Arsenal hapo Jumatano Usiku kwa Ziara ya
Mazoezi.
Baada ya Mechi hiyo na Arsenal, Man united hawana Mechi nyingine hadi baada ya Siku 10 watapoivaa Crystal Palace.