Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa, Mwaweje alikuwa akiifahamu vyema familia ya Chalz sambamba na mke wake (jina lipo) lakini hilo hakulijali na kumtokia mke wa Chalz ambaye kwa utamaduni wa Kiafrika ni shemejiye.
Chanzo cha habari kiliendelea kudai kuwa, ‘Mungu si Athuman wa Lucas’ siku isiyo na jina jamaa alimtumia ujumbe (SMS) mke wa mwenzake kwa kutumia maneno ya kumtoa nyoka pangoni kumbe muda huo bwana simu alikuwa nayo mwenye mke.
“Mume wangu, wala usikonde. Aliyetuma ujumbe huo si mwingine, ni Anton…”
Mume: “(akihamaki) Anton huyuhuyu?”
Mke: “Huyuhuyu mume wangu. Amekuwa akinitaka kimapenzi kwa muda mrefu sana, namkatalia lakini hasikii.”
Za mwizi 40: Bwana Anton John akiwa na pingu mkononi baada ya kunaswa na kamanda wa OFM pamoja na wanausalama.
“Sasa sikia, mkubalie,” mwanaume huyo alimwambia mke wake huku midomo ikimcheza kwa hasira.
Chini ya usimamizi wa mumewe, mwanamke huyo aliwasiliana na Anton na kumwambia alikuwa na nafasi wanaweza kukutana kwa ajili ya kumsaliti Chalz.
Baada ya kupata maelezo ya Chalz, mwandishi wa habari hii na Jeshi la Polisi Buguruni –Kwamnyamani jijini Dar na kuandaa mtego ambapo Jumatatu iliyopita, saa nane na ushee mchana, Anton ambaye naye inasemekana ana mke aliuingia mtego na kunasa kwenye chumba namba 5 akiwa na mke mwema huyo.
Ndani ya chumba hicho, Anton alikutwa na boksa tayari kwa mlo wa wizi ambao alibakia kuendelea kusikia njaa. Mezani, kulikuwa na chipsi kuku na pombe ambazo zingewapa stimu kabla ya mchezo.
Kitendo cha Chalz kumnasa jamaa huyo na mkewe kitandani kilimpandisha munkari ambapo nusura afanye ndivyo sivyo lakini alitulizwa na polisi waliokuwa eneo hilo kwa ajili kulinda usalama.
Kilichofuata baada ya hapo, mgoni huyo akiwa na pingu mkononi alipelekwa kwenye kituo hicho cha polisi ambapo awali, Chalz alitoa ripoti ya malalamiko baada ya kugundua jamaa huyo anataka kumtumbukiza mkewe kwenye mstari wa usaliti.
Taratibu za kisheria kuhusiana na kesi hiyo zilikuwa zikiendelea huku mgoni huyo akiwa chini ya ulinzi mkali.
source:GPL