NDOTO za Wazanzibari kuziona timu zao zikisonga mbele katika mashindano ya klabu barani Afrika, zimefutika kabisa baada ya jioni ya leo KMKM kutolewa katika kinyang’anyiro cha ligi ya mabingwa. Licha ya wanamaji hao kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dedebit FC ya Ethiopia katika pambano la marudiano lililochezwa uwanja wa Amaan, haikusaidia kuivusha timu hiyo zaidi ya kulinda heshima kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani.
Wachezaji wa KMKM na Dedebit wakionyeshana kazi leo Uwanja wa Amaan |
Mabingwa hao wa ligi kuu ya Zanzibar msimu uliopita, walianza kucheka na nyavu mapema katika dakika ya tatu ya mchezo, kwa bao lililofungwa na Maulid Kapenta baada ya kuwekewa pasi murua na Juma Mbwana. Bao hilo liliwafanya wachezaji wa timu hiyo waongeze kasi, lakini walishindwa kuzitumia nafasi nyingi za kufunga walizozipata katika kipindi cha kwanza.
Kocha wa KMKM, Ali Bushiri kushoto akisema na wachezaji wake wakati wa mechi leo Uwanja wa Amaan |