
Mwandishi Diana Bisangao wa matukiodaima.com Iringa
Mtu
mmoja jina bado halijafahamika mwenye umri kati ya miaka 60 hadi 70
amefariki dunia baada ya kugongwa na gari maeneo ya barabara kuu ya
Iringa - Mbeya.
Akizungumza
ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 26
februari majira ya saa 3:45 usiku.
Kamanda
Mungi aliitaja gari iliyomgonga marehemu ni aina ya Toyota Hiace yenye
namba za usajili T.731 AAU iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyejulikana
huku chanzo kikiwa ni mwendo kasi. Dereva anatafutwa.